Al Fajir
Bismillah Rahman Rahim. Assalm Aleykum.
Ewe mja tambua ya kwamba kila mmoja wetu ataonja umauti kama Mwenyenzi Mungu alivyosema katika Quran (Kur nafsi dhaaika tul mauti) hivyo basi tumia wakati ulionao kwa kujinyenyekeza mbele za Mola wako kwa kuswali, kutoa Dhaka, sadaka na mengineyo yanayompendeza Mwenyenzi Mungu. Milango ya Wafalme na Maraisi hufungwa ila Mlango wa Mwenyenzi Mungu upo wazi daima kwa ajili ya kuombwa. Tumuombe mwenyenzi Mungu atufanye miongoni mwa watakaoiona Pepo yake Tukufu. Amin.