SADAKA Network ni nini?
SADAKA network ni programu inayotoa vifaa vya kipekee vya teknolojia, vilivyo endelezwa/tengenezwa mahususi kwa ajili ya Waafrika, vilivyojumuisha tamaduni na fikra za mahala na kuzingatia hali ya teknolojia iliyopo ili kusaidia na kuwezesha jamii mbalimbali.
Moja wapo kifaa kilivyoendelezwa ni kilicho na ubora wa kipekee ulimwenguni, kifaa dhahiri cha uchangishaji fedha cha kidigitali kinachoweza kutumiwa na jamii tofauti za mahala ili kuchangia katika miradi ya jamii zao huku wakisaidiana na viongozi wao wa jamii na
SADAKA network.
Kusudi la SADAKA Network ni nini?
Mfumo wa
SADAKA network unawaruhusu viongozi wa jamii kuweza kuimarisha uhusiano wao na wafuatiliaji/wanaowaunga mkono/marafiki wao pia na jamii yao, kila siku; unawapatia njia rahisi na iliyo pana ya kusaidia miradi ya jamii zao, kuwezesha na kuimarisha riziki zao.
Pia viongozi wa jamii wanaweza kushirikisha taarifa na huduma zao kama vitabu vya kielektroniki, video, semina, vyeti, bidhaa, miradi na vingine vingi kwa halaiki bila haja ya nakala ngumu na usafirishaji hivyo kuwawezesha watu kupata huduma za haraka na zinazoaminika kutoka kwa viongozi wao wa jamii.
Ninaanza je/ vipi?
- Nenda kwenye ukurasa wa nyumbani wa tovuti www.sadakanetwork.com
- Chagua kiongozi wako wa jamii (Kiongozi wa Dini au Balozi)
- Kwenye listi itakayo jitokeza, chagua kiongozi wako wa jamii kisha bonyeza jina lake
- Ukishaingia kwenye kurasa binafsi ya kiongozi wako wa jamii, unaweza ukachagua huduma na taarifa unazozitaka
Kurasa ya Kiongozi wa Jamii – Unachohitaji kujua.
Kwenye kurasa hii unaweza ukapata taarifa na huduma za kiongozi wa jamii (picha, video, matukio na huduma).
Huduma
- MWANACHAMA/MFUATILIAJI (/RAFIKI/MFUAS)
Utakapo bonyeza kitufe cha MWANACHAMA au MFUATILIAJI kwenye kurasa ya kiongozi wa jamii SADAKA network itakuruhusu uwe mwanachama wa jamii (baada ya kujisajili), utaona na kunufaika na huduma maalum na faida za WAFUATILIAJI na WANACHAMA.
- BARAKA/MUONGOZO
Utakapo bonyeza kitufe cha BARAKA/MUONGOZO kwenye kurasa ya kiongozi wa jamii SADAKA network utakuruhusu unufaike na Baraka na Miongozo ya mara kwa mara kutoka kwa viongozi wa dini kwa kutoa sadaka/fedha ya kiwango chochote nafsi yako itavyoridhia.
- CHANGIA
Utakapo bonyeza kitufe cha CHANGIA kwenye kurasa ya kiongozi wa jamii SADAKA network itakupa njia rahisi ya kuchangia kwenye mradi wa jamii uliopo chini ya kiongozi wa jamii, kwa kuchagua baina ya mradi mmoja wapo au zaidi inayopatikana na kusaidia miradi itakayo nufaisha jamii yako.
- MAOMBI
Utakapo bonyeza kitufe cha MAOMBI kwenye kurasa ya kiongozi wa jamii SADAKA network itakupa njia rahisi ya kuomba MAOMBI MAALUMU sawasawa na chaguo lako kutoka kwa viongozi wa dini ili litumwe kwa watu wako unaowapenda kwa kuchagua maombi/dua moja wapo kati ya hayo yaliopo katika kurasa. Kisga kiongozi wa dini aliyochaguliwa atapokea ombi hili na kumuombea huyo mtu kama ulivyagiza.
- GHALA
Utakapo bonyeza kitufe cha GHALA kwenye kurasa ya kiongozi wa jamii SADAKA network itakuruhusu uingie kwenye ghala binafsi ya kiongozi wa jamii na kuweza kuona vitabu vya kwenye mtandao, semina, bidhaa, vyeti na zaidi. Namna ya pekee ya kukuwezesha kuchagua kwenye listi ya GHALA ni kwa kuwa mwanachama au mfuatiliaji wa kiongozi wa jamii.
Ninawezaje kuwa MWANACHAMA/MFUATILIAJI?
Baada ya kumchagua kiongozi wa jamii, ingia kwenye kurasa yake binafsi kisha bonyeza MWANACHAMA, hapa unakuta taarifa utatakiwa kujaza ili uwe MWANACHAMA/MFUATILIAJI wa kiongozi wako wa jamii na utaona shughuli zote za jamii na utaweza kupata faida na huduma maalumu za jamii.
Je huduma BARAKA/MUONGOZO ya inafanyaje kazi?
Baada ya kumchagua kiongozi wa jamii, ingia kwenye kurasa yake binafsi kisha bonyeza BARAKA, kwenye kurasa ya BARAKA utakuta kadhaa za ujumbe wa baraka/miongozo za kuchagua kama sehemu yako ya kuchangia na kusaidia mara kwa mara.
Je huduma CHANGIA ya inafanyaje kazi?
Baada ya kumchagua kiongozi wa jamii, ingia kwenye kurasa yake binafsi kisha bonyeza CHANGIA, kwenye kurasa ya CHANGIA utakuta miradi ya jamii tofauti ya kuchagua. Kwa kubonyeza kwenye mradi wa jamii unaoutaka, utakuta video na picha zenye maelezo kuhusu mradi uliochaguliwa.
Utaweza kutoa msaada kwa kuchangia kwenye kwenye mradi wa jamii uliochagua.
Je huduma MAOMBI ya inafanyaje kazi?
Baada ya kumchagua kiongozi wa jamii, ingia kwenye kurasa yake binafsi kisha bonyeza MAOMBI, kwenye kurasa ya MAOMBI utakuta maombi tofauti ya kuchagua. Kwa kubonyeza kwenye maombi unayoyataka utakuta video zenye maelezo kuhusu maombi/dua na utaweza kumuomba kiongozi wa dini kuwaombea wale uwapendao kwenye saa yao ya uhitaji sawasawa na maombi/dua uliyochagua.
Wapendwa wako watapokea ujumbe utakao wafahamisha kuwa kiongozi wako wa dini anafanya maombi kwa ajili yao kama ulivyoomba.
Huduma hii inapatikana kwenye kurasa ya viongozi wa dini.
Je huduma GHALA ya inafanyaje kazi?
Baada ya kumchagua kiongozi wa jamii, ingia kwenye kurasa yake binafsi kisha bonyeza GHALA, kwenye kurasa ya GHALA utaona taarifa na binafsi na bidhaa na utaona vitu alivyovitengeneza.
Kwa kubonyeza kitufe na kuchagu bidhaa unayotaka , utaweza kupakua taarifa binafsi za kiongozi wako wa jamii au kuagizia bidhaa zake binafsi kupitia mtandao wa intaneti.
Unaweza kufaidi huduma hizi endapo tu wewe ni MWANACHAMA.
Je ninawezaje kushirikisha watu wengine kwenye matumizi ya huduma za SADAKA Network?
Kile unachohitajika kufanya ni kuwaeleza/kuwapatia ndugu na marafiki kiungo cha tovuti
www.sadakanetwork.com au kodi ya USSD
*150*92# ili waweze kutumia na kufaidi huduma za
SADAKA network na kusaidia jamii tofauti muda wowote wanaotaka.
Je ninaweza kutumia SADAKA Network kupitia simu yangu ya mkononi?
NDIO! unaweza kufaidi huduma za
SADAKA network zinazopatikana kwenye mtandao wa intaneti kupitia kyomyuta, kompyuta bapa na sikanu (simu zinawoza kutumia intaneti) kupitia tovuti yetu
www.sadakanetwork.com ya pia kupitia simu za kawaida zisizoweza kutumia intaneti kupitia au kodi ya USSD
*150*92#
Je SADAKA Network inafanya kazi kimataifa?
Huduma za
SADAKA network zinapatikana kwenye kila nchi ijapokuwa uchangiaji wa fedha kwa simu za mkononi kupitia (M-pesa & Tigo pesa) unapatikana Tanzania tu.
Je SADAKA Network unasaidia miradi gani?
SADAKA network ni programu dhahiri inayotoa uwezo kwa jamii tofauti iliziweze kutengeneza, kuchangia na kutoa msaada miradi yoyote wanayotamani kujishirikisha nayo kwa manufaa ya jamii.
Je ninaweza kuwasiliana na kiongozi wangu wa jamii kabla ya kutumia SADAKA Network?
Ndio, unaouhuru wa kuwasiliana na kiongozi wako wa jamii kabla na baada ya kutumia
SADAKA network maana inatoa huduma kwa ajili yako wewe na kiongozi wako wa jamii.Ukimkuta kiongozi wa jamii kwenye mfumo wa mtandao wetu inamaana kuwa wao pia wanautumia ili waweze kusaidia jamii na wafuatiliaji wao waweze kuwapata.
Je ninaweza kuuchangia mradi uliopo chini ya kiongozi yoyote wa jamii?
SADAKA network inashirikiana na viongozi wa jamii wengi. Unaweza kuichangia miradi iliyopo chini ya kiongozi yoyote wa jamii kadiri ya moyo wako utakavyopenda ilimradi tu, uwepo kwenye mfumo wa mtandao wetu.
Je nitapokea kihibitisho cha micango yangu?
SADAKA network itakutumia ujumbe au barua pepe yeye kithibitisho baada ya kutoa mchango wowote au kutumuia huduma yoyote kupitia mtandao wetu, pia kwa wale wanaotumia huduma za mitandao ya simu watapokea ujumbe wa makato ya malipo yaliyofanyika.