Usinichukulie poa
Mboni A. Masimba (Namba ya Utambulisho: Y0010)
Mkurugenzi

SADAKA network washerekea siku ya kuzaliwa ya Mmoja wa timu yao pamoja na watoto yatima wa kituo cha Umra na dada Mboni Masimba.
Feb 13, 2019

Mradi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Urma

Disemba ya mwaka uliopita tulichukua hatua ya kujifunza kuhusu vituo vya watoto yatima na namna vinaendeshwa hapa nchini. Tulitaka kuona kwa macho yetu hali ya watoto yatima na hali ya vituo watoto wanapoishi. Ukweli, ni mengi tuliyogundua kwa mfano maeneo, hali ya vituo na masiha yao ya kila siku.
Kituo cha Watoto Yatima cha Urma ni nyumbani kwa watoto yatima zaidi ya 200. Wanazo nyumba nne hapa Dar es Salama ambazo zote zimejaa watoto yatima. Wakati wa kipindi cha siku za likizo za Krismasi tulikutana na meneja na alitudadavulia jinsi maisha yao yanavyoenda katika kipindi cha mwaka mmoja, matatizo na jinsi jamii inavyowasaidia.
Tulijifunza kuwa vifaa vya kuandikia kwa ajili ya shule ni moja wapo ya vitu wanavyohitaji haswa katika msimu wa kurudi shule sanasana kipindi mwaka unapoanza pamoja na nguo kwa ajili ya baadhi ya watoto. Baada ya kupata taarifa hizi, tulitambua kuwa iibidi tuwapatie msaada haswa katika kipindi shule zinapofunguliwa. Na kama tulivyo jaliwa, kweli kulikuwa na msaada tulioweza kuuotoa.
Hapa SADAKA Network tunapenda kusherekea siku za kuzaliwa za wafanyakazi wenzetu na kwa bahati nzuri siku ya kuzaliwa ya bosi wetu Mr. Tamir ilikuwa mwezi wa januari, hivyo basi tuliamua kusherekea siku hiyo ya furaha kwake pamoja na watoto yatima wa kituo cha Umra. Tuiwanunuia vifaa vya kuandikia, sabuni za kufuia/kusafishia na kukusanya nguo kutoka kwa marafiki na wafanyakazi wenzetu waliyokuwa tayari kufanya fadhila badala ya kuzitupa. Katika misioni yetu ya kutoa msaada kwa kituo cha watoto yatima Urma, tulifurahia kuungwa mkono na Dada Mboni aliyekuwa amezindua duka a mabegi katika siku za karibuni kwa niaba ya mtoto wake wa kiume. Mtoto huyu alitushangaza na kutufurahisha alipokuwa tayari kujumuika nasi katika safari yetu nzuri pamoja na kituo cha Umra.
Mchana wa Ijumaa tuliwatembelea watoto yatima wa kituo cha Umra kilichopo Mikumi Magomeni na mapokezi tuiyopata yaitufurahisha mno.Tabasamu kwenye nyuso zao ziligusa mioyo yetu na tulifurahia kabisa kuamua kushinda nao siku hiyo. Hapo awali tulikuwa tumeandaa mlo wa mchana kabla ya kuwatembelea pia tulinunua keki kwa ajili ya sherere ya siku ya kuzaliwa. Tulikula hadi kutosheka na kusherekea kwa pamoja katika siku hii nzuri ambayo bosi wetu aliamua kuwajumuisha/kusherekea nao. Tuliwapa zawadi tulizo waletea na walikuwa wenye furaha mno na kushukuru kwa ajili ya tuliyo watendea.
Tukio hii lilikuwa la kipekee sana na mengine mengi yanakuja, SADAKA Network imeweka kipaumbele kwenye kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika jamii zetu na kuwasihi/kushirikisha wanajamii kufanya hivyo pia kwa kutumia rasilimai zilizopo.
Nitanukuu maneno ya moja wapo ya waandishi tunaowapenda “maisha hujayaishi mpaka tu utakapo mfanyia mtu kitu asichoweza kukulipa”. Haya ni maneno ambayo SADAKA Network yanatamani si tu kuyatimiza kila siku bali hata kufaana nayo kila siku!