"Watendee wengine kama wewe upendavyo kutendewa"
Layla (Voice Fairy) (Namba ya Utambulisho: Y0012)
Mwanamuziki

Rudisha tabasamu usoni mwao 2019 kwenye UDSM bonanza
Jun 29, 2019

Mchezo ni lugha ya kimataifa. Mara nyingi huonekana kama aina ya burudani au uajiri (kwa wachezaji), ila ukweli ni kwamba mchezo, ingawa hili si dhahiri, unalenga na unatumika kwa ajili ya kufanikisha madhumuni mengine, moja kati ya hayo ni kuleta/kuendeleza amani. La mwisho (miongoni mwa yaliyotajwa) kuwa lenye umuhimu mkubwa katika jamii zenye machafuko/mafarakano/vurugu; michezo inaweza ikatumika. Katika ubora wake, michezo inaweza kuleta umoja baina ya watu, bila kujali asili yao, historia, imani ya kidini au hali ya kiuchumi. Lugha hii ya kimataifa pia ina uwezo wa kuwaleta watu pamoja ili waweze kujadili maswala mbalimbali yanayoendelea ndani ya jamii.
Chuo Kikuu cha Dar es Salama waliandaa onyesho la kimchezo kama njia ya kuleta pamoja watu waliowahi kusoma hapo, kama njia ya kuwatia moyo wale waliopo masomoni. Michezo tofauti ilichezwa kati ya alumni na wanafunzi/waliopo masomoni.
Sisi, SADAKA Network tulikuwa washiriki katika onyesho hilo na tuliweza kueleza umati kuhusu mradi/ushirika wetu na hospitali ya Aga Khan, hospitali ya taifa Muhimbili na Women Reconstructive International.
Tuliweza kuongelea maswala ya ukatili wa kijinsia majumbani na athari yake katika jamii. Pia tuliongelea kuhusu upasuaji wa kurekebisha utakaofanyika mwezi wa nane na wa kumi ili waweze kuwafahamisha ndugu na marafiki ambao wanamakovu na wanaweza kunufaika na upasuaji wa aina hii.
Tungependa kukishukuru Chuo Kikuu cha Dar es Salama kwa kutupa fursa hii nzuri pamoja na wanafunzi wanaoendelea kuweka picha za onyesho kwenye mitandao ya kijamii.
Pamoja tunaweza kurudisha tabasamu kwenye sura za waathirika wa ukatili wa kijinsia.