Sound of Africa
Radio Free Africa (Namba ya Utambulisho: C0016)
Radio Station
Radio Free Africa (Namba ya Utambulisho: C0016)
Radio Station

Ujumbe Binafsi

RFA Sauti ya Afrika.Makao makuu Mwanza,Redio inayosikika Tanzania nzima,Afrika mashariki & kati, maziwa makuu Na Duniani. Inaongoza kwa Habari Elimu na Burudani

Miradi

Timu ya SADAKA Network kuwatembelea waathirika wa majanga ya moto na ukatili Majumbani baada ya kufanyiwa upasuaji.
Aug 16, 2019


Timu ya SADAKA network ilipata nafasi ya kuwatembelea waathirika wa majanga yatokeayo majumbani pamoja na ukatili baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa bandaji Aga khan hospital ikiwa ni miongoni mwa mradi wa “ rudisha tabasamu usoni mwao” ili kuwafariji, na kuwapatia zawadi ya mafuta “ Vaseline skin creams” yaliyotolewa na Unilever Tanzania ili kurahisisha uponaji wao.
Tunatoa shukrani kwa wabia wetu, Aga khan Hospital, RWI foundation, Muhimbili National Hospital, Unilever, Mai ... Soma Zaidi...

Mkutano na waandishi wa habari kwaajili ya Mradi wa "Rudisha tabasamu usoni mwao"2019
Aug 15, 2019

Timu ya SADAKA network pamoja na madaktari kutoka Aga khan hospital, Muhimbili hospital na wabia wetu MAI consultation waliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kutoa taarifa kuhusu mradi unaoendelea wa "Rudisha tabasamu usoni mwao" ambao lengo lake kuu ni kuwafanyia upasuaji wa marekebisho wanawake na watoto waliopata majeraha kutokana na ajali na ukatili majumbani.
Mradi wa "Rudisha tabasamu usoni mwao"unafanyika katika makundi mawili ili kukamilisha idadi ya waathirika wote 100. Kundi ... Soma Zaidi...

Rudisha tabasamu usoni mwao kwenye TOT Bonanza na SADAKA angels.
Jul 27, 2019

Ilikuwa tarehe 27/07/2019 ambapo TOT BONANZA lilifanyika katika viwanja vya Posta kijitonyama iliyoanza kwa mashindano ya mbio mapema saa 12 asubuhi. Watu wachache walifanikiwa kufika mapema huku wengine walifika baadae saa 4 asubuhi. Michezo ilifurahisha kwasababu kulikuwa na washiriki wengi kama wajasiriamali, wanamichezo na washangiliaji SADAKA network pia tulikuwepo. Washiriki walipata nafasi ya kujionea mambo mapya na marafiki. Kila kitu kilichofanyika siku hiyo kilikuwa cha kufurahisha ... Soma Zaidi...

Rudisha tabasamu usoni mwao -Kambi ya uchunguzi Aga khan 2019
Jul 13, 2019


IIlikua tarehe 13 julai 2019 timu ya sadaka network tulifika agakhan hospitali tayari kwakunzana sehemu ya kwanza ya mradi wa kurudisha tabasamu usoni mwa waathirika wa ajali za moto na vurungu za majumbani.
Tunashukuru sana kwakua muitikio ulikua mkubwa watu wengi walifika kwajili ya uchunguzi wa awali Watoto na wanawake walifika kwa wingi kutoka sehemu tofauti tofauti. Kama timu, tuliungana na madaktari kutoka Agakhan na Muhimbili hospitali kwa pamoja tulishirikana kuwa hudumia ... Soma Zaidi...

Rudisha tabasamu usoni mwao 2019 kwenye UDSM bonanza
Jun 29, 2019

Mchezo ni lugha ya kimataifa. Mara nyingi huonekana kama aina ya burudani au uajiri (kwa wachezaji), ila ukweli ni kwamba mchezo, ingawa hili si dhahiri, unalenga na unatumika kwa ajili ya kufanikisha madhumuni mengine, moja kati ya hayo ni kuleta/kuendeleza amani. La mwisho (miongoni mwa yaliyotajwa) kuwa lenye umuhimu mkubwa katika jamii zenye machafuko/mafarakano/vurugu; michezo inaweza ikatumika. Katika ubora wake, michezo inaweza kuleta umoja baina ya watu, bila kujali asili yao, ... Soma Zaidi...

Rudisha tabasamu usoni mwao -kambi ya uchunguzi kisarawe.
Jun 29, 2019

Mradi wa “ Rudisha tabasamu kwenye nyuso zao" unadhumuni la kuwafanyia upasuaji wa kurekebisha wanawake na watoto nchini Tanzania. Kama sehemu ya mradi huu tuliamua kutembelea wilaya ya Kisarawe kwa kusudi la kuweka kambi ya uchunguzi ya kutafuta wanawake na watoto wenye makovu na yaliyo sababishwa na ajali, ajali za moto na ukatili wa kijinsia.
Tulifika Kisarawe Jumamosi asubuhi tarehe 29/06/2014 pamoja na madaktari kutoka Hospitali ya Aga Khan na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na klabu ya ... Soma Zaidi...

Jiandikishe bure

Wafuasi

Changia mradi ya jumuiya

CHANGIA

Onyesha huduma zote

Huduma zote