Muziki Unaongea
EFM . (Namba ya Utambulisho: C0006)
kituo cha radio

Rudisha tabasamu usoni mwao -Kambi ya uchunguzi Aga khan 2019
Jul 13, 2019


IIlikua tarehe 13 julai 2019 timu ya sadaka network tulifika agakhan hospitali tayari kwakunzana sehemu ya kwanza ya mradi wa kurudisha tabasamu usoni mwa waathirika wa ajali za moto na vurungu za majumbani.
Tunashukuru sana kwakua muitikio ulikua mkubwa watu wengi walifika kwajili ya uchunguzi wa awali Watoto na wanawake walifika kwa wingi kutoka sehemu tofauti tofauti. Kama timu, tuliungana na madaktari kutoka Agakhan na Muhimbili hospitali kwa pamoja tulishirikana kuwa hudumia waathirika wote wenye makovo na majeraha.
Tunamshukuru Mungu zoezi lilifanikiwa kikamilifu na baadhi ya waathirika walifanikiwa kupata nafasi.