Muziki Unaongea
EFM . (Namba ya Utambulisho: C0006)
kituo cha radio

Rudisha tabasamu usoni mwao -kambi ya uchunguzi kisarawe.
Jun 29, 2019

Mradi wa “ Rudisha tabasamu kwenye nyuso zao" unadhumuni la kuwafanyia upasuaji wa kurekebisha wanawake na watoto nchini Tanzania. Kama sehemu ya mradi huu tuliamua kutembelea wilaya ya Kisarawe kwa kusudi la kuweka kambi ya uchunguzi ya kutafuta wanawake na watoto wenye makovu na yaliyo sababishwa na ajali, ajali za moto na ukatili wa kijinsia.
Tulifika Kisarawe Jumamosi asubuhi tarehe 29/06/2014 pamoja na madaktari kutoka Hospitali ya Aga Khan na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na klabu ya Rotary ya Peninsula, Dar es Salaam. Sisi sote tulikuwa tayari kushiriki na kuwapokea wanawake na watoto watakao tokea kwa ajili ya uchunguzi.
Ilikuwa siku nzuri ambayo tuliweza kupata wanawake ambao walikuja kufanyiwa uchunguzi na ni wawili ambao walistahili kufanyiwa upasuaji.
Tungependa kumshukuru kila mtu aliyefanya tukio hili liwezekane, kwa muda wao na ushiriki wao.