uongozi ni utumishi
Askofu Nickson J. Kalinga (Namba ya Utambulisho: R0031)
Askofu
Bethel river of life (Stanley sec school)
Dar es Salaam, Temeke, Dar es salaam
Tanzania

Sala ya mafanikio ya elimu

Sote tunafahamu kwamba elimu ni ufunguo wa maisha. Kwa sababu hii, wazazi wanafanya kazi kwa bidii ili kuweza kuwapeleka watoto wao shule na pia watu wazima wanajiendeleza kielimu kwa kusoma masomo ya elimu ya juu ili kuweza kuongeza mwanga kwenye kazi zao. Hata hivyo, elimu haitakuwa na maana endapo Mungu atasahaulika. Ili kuweza kufanikiwa kielimu, mtu anahitaji muongozo wa Mungu ili afanye uchaguzi sahihi wa kazi.