Waambie wana wa Israel wasonge mbele
Jackson S. Jackson (Namba ya Utambulisho: P0002)
Askofu

SADAKA NETWORK,AGAKHAN NA HOPITAL YA MUHIMBILI KUUNGANA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA
Nov 08, 2018

Watanzania wameombwa kwa pamoja kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya SADAKA NETWORK , Hospitali ya Muhimbili na Aga Khan kwa kushirikiana na Women to women foundation kuchangia kurudisha tabasamu usoni kwa wakina mama na watoto waliopata matatizo hayo kwa bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia, kupigwa au matatizo yoyote yaliyopelekea wao kuharibika maumbile yao ikiwa ni usoni ama sehemu nyengine ya mwili.

Mwanzilishi wa taasisi hiyo Dkt. Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa gharama za kuwatibu watoto na akina mama ni kubwa na haziwezi kubebwa na Muhimbili au Aga Khan peke yake wala Women to women foundation,bali ghalama hizi zitafanikiwa endapo wananchi wataungana kwa pamoja ili kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi hilo.

"Upasuaji huu utafanyika katika Hospitali ya Muhimbili na Aga Khan na tunatarajia kuwafanyia upasuaji watu 40 kutoka sehemu zote Tanzania,hivyo pesa inayohitajika ni Tsh Milioni 268" alisema Dkt. Msengi.