SADAKA Network ikishirikiana na ubalozi wa Israel nchini Kenya yaunga mkono mradi wa 'Tokomeza zero' Wilaya ya kisarawe, Tanzania
May 06, 2019

Vitabu ni maarifa na maarifa ni nguvu, fikiria kama kila mtoto Afrika angekuwa na uwezo wa kupata vitabu, vya somo la aina lolote analotamani, mahali anapoweza kujifunza na kupanua ubunifu kila waendapo shule tofauti na masomo ya kila siku.
Mwanzoni mwa Mei 2019, SADAKA network ilipokea mchango wa vitabu 250 vya masomo tofauti vilivyopo katika lugha ya Kingereza kutoka Ubalozi wa Israeli, Nairobi, maana wao ni miongoni ya wafadhili wa miradi yetu ya kijamii ndani ya Afrika.
Tarehe 6 ya mwezi Mei SADAKA network ilienda Wilayani Kisarawe, Tanzania, na kutoa msaada wa vitabu 150 kwenye ofisi ya Wilaya ili kufadhili kampeni ya “Tokomeza Zero”.
https://www.ippmedia.com/en/news/kisarawe%C2%A0raises-915m-improvement-district’s-education (EN)
http://www.dar24.com/bonta-afafanua-kilio-chake-kwa-dc-jokate-kuhusu-wimbo-wa-tokomeza-zero/ (KW)
Kitovu cha hii kampeni ni kuwezesha kielimu watoto wa kike ndani ya wilaya hiyo (Kisarawe) inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Jokate Mwegelo.
Hii kampeni inafanya juhudi kufadhili na kuinua elimu baina ya watoto wa kike ndani ya wilaya hiyo, ambapo lengo ni kutokomeza matokeo ya chini baina ya wanafunzi wa Kisarawe.
Tangia kampeni hiyo ilipoanza, matokeo ya wanafunzi wa wilaya hiyo yameanza kutengemaa na idadi ya wanafunzi wenye divisheni ziro zimepungua.
Tunakaribisha kila mtu kuungana na kusaidia kwa namna yoyote inayowezekana ili kuinua wanafunzi wengi iwezekanavyo na kuifadhili kampeni ya “Tokomeza Zero”
“Kitabu kimoja, Mtoto mmoja… “