“Kitabu kimoja, Mtoto mmoja" kutembelea Oysterbay shule ya msingi Dar es Salaam
May 10, 2019

Vitabu ni maarifa na maarifa ni nguvu, fikiria kama kila mtoto Afrika angekuwa na uwezo wa kupata vitabu, vya somo la aina lolote analotamani, mahali anapoweza kujifunza na kupanua ubunifu kila waendapo shule tofauti na masomo ya kila siku.
Mwanzoni mwa Mei 2019, SADAKA network ilipokea mchango wa vitabu 250 vya masomo tofauti vilivyopo katika lugha ya Kingereza kutoka Ubalozi wa Israeli, Nairobi, maana wao ni miongoni ya wafadhili wa miradi yetu ya kijamii ndani ya Afrika.
Tarehe 10 ya mwezi Mei SADAKA network ilienda Shule ya Msingi Oysterbay, ya Dar es Salaam, na kutoa msaada wa vitabu 100 kwenye maktaba ya shule ili wanafunzi wawe na nyenzo za kujifunzia za masomo tofautI.
Tunakaribisha kila mtu kuungana na kusaidia kwa namna yoyote inayowezekana ili kuinua wanafunzi wengi iwezekanavyo na kuifadhili kampeni ya “Kitabu kimoja, Mtoto mmoja… “