Muigizaji/Muandaaji Monalisa .
Namba ya Utambulisho: Y0003

SADAKA NETWORK,AGAKHAN NA HOPITAL YA MUHIMBILI KUUNGANA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA
Nov 08, 2018

Nenda kwenye Mradi

Nelson Mandela aliwahi kusema kwamba katika maisha jambo lililo na maana zaidi si kuishi tu. Bali ni utofauti tunaouwezesha kutokea katika maisha ya wengine ndio
unaongeza maana katika maisha tunayoishi. Binafsi naguswa na maneno haya na naamini tuko hapa duniani kwa makusudio makubwa zaidi ya kutafuta ili kupata kile
tunachokitaka katika maisha. Makusudio hayo kwangu ni kuona Wanawake na Watoto ambao ni waathirika wa vitendo mbali mbali dhalili katika jamii yetu, majanga ya asili,
ajali na wale wanaozaliwa wakiwa na changamoto mbali mbali za kimaumbile wanapata fursa ya kutabasamu tena. Huo ndio utofauti ninaoutamani kuuona unatokea. Tafadhali jumuika nami.