Al Fajir
Changamoto ni sehemu ya maisha yetu,lakini kamwe zisikukatishe tamaa kuwepo kwako hapa duniani, kwani huu ni mpango kamili wa mwenyeezi mungu, hukuja duniani kwa bahati mbaya bali ni kwa lengo maalumu ambalo ni kumuabudu mwenyeezi mungu, hivyo kuwepo kwako hapa duniani hakikisha unalitambua lengo hilo na kulitimiza, haijalishi unapitia kwenye wakati gani kwa sasa, katika sura ya (51) aya ya (56) mwenyeezi mungu amesema; (SIKUWAUMBA MAJINI NA WATU, ILA WANIABUDU MIMI).