KUHUSU SISI

Tupo hapa sio tu kuwapatia jukwaa, tupo hapa kutengeneza jamii!

 

Maendeleo ya kijamii  ni muhimu kwenye kila jamii, Jamii ikipewa vifaa muhimu na jukwaa maalumu, malengo muhimu yanaweza kufikiwa au kupatikana, Hivyo basi ni muhimu kuvunja vikwazo vyote vinavyozuia jamii kujikwamua nakutambulisha njia mbadala zitakazofanikisha mawasiliano kati ya jamii na viongozi wake.

SADAKA network inatoa vifaa vya kipekee vya teknolojia, vilivyo tengenezwa kwa kuipa umuhimu mahala husika, mahususi kwa ajili ya wananchi, vilitengenezwa kwa jumuisha tamaduni na fikra za mahala na kuzingatia hali ya teknolojia iliyopo ili kusaidia na kuwezesha jamii mbalimbali; huku kipaumbele ikiwa kwa vijana, ili wasimamie na kuwajibika kwaajili ya maisha yao ya baadaye, kwa kuwapatia maarifa, miongozo na vifaa sahihi (namna ya kuanzisha mradi, kurasimisha mpango wa biashara, kuandaa na kusimamia bajeti, mahusiano na wachuuzi, mahusiano na wafadhili, masoko n.k) ili kutekeleza kwa mafanikio miradi ya jamii mbalimbali hadi mpaka ikamilike, ikiwa chini ya usimamizi wa SADAKA network

Moja wapo wa uboreshaji huo ni kifaa cha kidigitali, cha uchangishaji fedha chenye ubora wa kipekee ulimwenguni, kitakacho boresha uwazi (kujua taarifa za mradi na mpango wa  matumizi ya fedha zilizochangishwa, kiasi cha fedha zinazohitajika, wabia wa mradi, malengo ya miradi, kupokea ripoti za maendeleo na mafanikio ya miradi hata mpaka kikomo cha mradi husika) kinachoweza kutumiwa na jamii ya mahala kuchangia na kuchangisha fedha kutoka kwa jamii mbalimbali ndani ya nchi, kwa ajili ya miradi yao husika huku wakisaidiana na viongozi wao wa jamii na SADAKA network.

SADAKA network itasimamia miradi na kuhusisha vijana kutoka kwenye jamii kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
Mfumo huu huleta uwazi na uwajibikaji juu ya kipengele cha kifedha cha miradi, ambavyo hujenga ustahilifu na uaminifu kati ya wafadhili, jamii na viongozi wake wa kijamii kuelekea kwenye lengo moja.

Tunaimani kwamba kwa kutumia njia hii ya kuwezesha vijana na jamii zao kushiriki kama sehemu ya utendaji katika kuanzisha na kusimamia miradi yao ya kijamii, tunaweza kutengeneza athari kubwa na endelevu ambazo zitaboresha kwa kiasi kikubwa maisha ya jamii nyingi ndani ya Afrika.

 

Mpe mtu samaki utamlisha kwa siku;

                                               Mfundishe jinsi ya kuvua na utamlisha maisha yote

 

 

Dhamira Yetu

Kusaidia jamii ndani ya Afrika kupitia viongozi wao wa jamii, kwa kuwapatia zana sahihi za kiteknolojia na muongozo kuanzisha na kusimamia miradi yao ya kijamii, kwa kuwezesha na kuwafundisha vijana kuongoza mabadiliko hayo.

 

Dira Yetu

Kuwa na jamii nyingi endelevu ndani ya Afrika, ambazo zitaweza kuanzisha, kusimamia na kusaidia miradi yao ya kijamii na kuboresha maisha yao kwa kuwa na umiliki na kuwajibika kwa maisha yao ya baadaye.