Mukhtasari
"Rudisha tabasamu usoni mwao” ni mpango endelevu chini ya Reconstructing Women International programu ya International Society for Plastic Reconstructive Aesthetic Surgery wakishirikiana na hospitali ya Aga Khan na hospitali ya taifa Muhimbili.
Kampeni hii imelenga kurudisha tabasamu kwenye nyuso za wahanga wa ajali na ukatili wa kijinsia ambao umewaachia makovu si tu ya kimwili bali hata kiakili, kwa kuchangisha fedha ambazo zinatumika kwenye utoaji wa upasuaji wa urekebishaji kwa wahanga hao.
Ukatili wa kijinsia ni fedheha ya taifa ambayo serikali inachukua hatua za kulitatua. Ijapokuwa hakuna sera au miongozo kwa ajili ya ukatili wa kijinsia, serikali imechukua hatua za kutengeneza misingi imara ya kuzuia na kushughulikia ukatili wa kijinsia kama ilivyo dhahiri na sera na mikakati inayotetea usawa wa kijinsia.
Taasisi ya , Reconstructing Women International kwa miaka mitatu inaingia minne sasa imekuwa ikifanya kazi pamoja na hospitali ya Aga Khan na hospitali ya taifa Muhimbili kutoa upasuaji wa urekebishaji kwa wahanga wa ajali na ukatili wa kijinsia, waathiriwa wa ukatili wa kimwili na majanga ya moto hata wakapata ulemavu au kubaki na makovu.
Shirika la kutoa msaada la Reconstructing Women International lililopo Marekani na Canada linafadhiliwa na wapasuaji wa urekebishaji wa kike, na lengo lake ni kusaidia wanawake na watoto wanaotaabishwa na majeraha yalioacha ulemavu au yanayofanya watengwe na jamii na kuwapa kiwewe ili waendelee kuishi maisha yenye furaha na yaliyostawi. Na uzatiti wa kutotoa misaada katika nchi mbalimbali za Afrika, Reconstructing Women International wameungana na hospitali ya taifa Muhimbili na hospitali ya Aga Khan ili kuendeleza utoaji wa huduma kwa wahanga wa ajali na ukatili wa kijinsia nchini.
Hospitali ya taifa Muhimbili na ya Aga Khan itatoa madaktari, mahala na vifaa kwa ajili ya taratibu zote. Kusudi ni kuisaidia Reconstructing Women International na wabia wake kuongeza uelewa na kuchangisha fedha, kwa ajili ya kuendeleza mpango huu, kupitia SADAKA Network wa kuchangisha fedha na kuhuluku habari kuhusu kazi nzuri hizi shirika zinafanya. Kwa kutumia kifaa chetu cha kipekee ulimwenguni na chenye unyofu kinachoweza kutumika na jamii zetu kuchangisha fedha katika jamii tofauti nchini kwa ajili ya miradi ya jamii zao kwa msaada wa viongozi wa jamii na SADAKA network.
Hapa tunahainisha haja ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendeleza huu mpango na kuhuluku habari kuhusu mpango huo pia. Lengo ni kutibu wahanga wengi wa ajali na ukatili wa kijinsia ili waweze kuwa na hali ya kawaida kama ilivyokuwa awali licha ya mambo yaliosababisha hata wakawa wahanga. *