Muziki Unaongea
EFM . (Namba ya Utambulisho: C0006)
kituo cha radio

Mkutano na waandishi wa habari kwaajili ya Mradi wa "Rudisha tabasamu usoni mwao"2019
Aug 15, 2019

Timu ya SADAKA network pamoja na madaktari kutoka Aga khan hospital, Muhimbili hospital na wabia wetu MAI consultation waliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kutoa taarifa kuhusu mradi unaoendelea wa "Rudisha tabasamu usoni mwao" ambao lengo lake kuu ni kuwafanyia upasuaji wa marekebisho wanawake na watoto waliopata majeraha kutokana na ajali na ukatili majumbani.
Mradi wa "Rudisha tabasamu usoni mwao"unafanyika katika makundi mawili ili kukamilisha idadi ya waathirika wote 100. Kundi la kwanza linafanyika mwezi huu wa nane na jumla ya waathirika 50 tayari wako hospital kwaajili ya upasuaji huo, kundi la pili litafanyika mwezi wa 12 kwa ajili ya waathirika wengine 50.
Upasuaji huu unafanyika katika hospitali ya Aga khan na madaktari kutoka Muhimbili na shirika la wanawake madaktari wa upasuaji kutoka Canada na Marekani.
Vyombo na waandishi wa habari mbalimbali waliofanikiwa kufika walipata nafasi ya kupata taarifa kuhusu idadi kamili ya waathirika waliotayari hospitali na wanaendelea na upasuaji ambao wanafanya jumla ya idadi ya 50 kulingana na kundi la kwanza (mwezi wa nane) na wote wanaendelea vizuri. Tunawaombea wapate nafuu haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa mabalozi, wabia na jamii kwa ujumla kwa ushirikiano wenu mlioutoa ili kuweza kufanikisha mradi huu.