TUMUOGOPE MWENYEZI MUNGU
Shekhe Zailai H. Mkoyogore (Namba ya Utambulisho: A0007)
Sheikh wa wilaya ya temeke
Masjid Kadiria (karibu na Temeke hospital)
Dar es Salaam, Temeke, Dar es salaam
Tanzania

Sheikh Zailai Mkoyogore - Cheti Binafsi (Kiswahili)

Assalaam Aleykum

Biashara kubwa Duniani ni kusoma Quran, kudumisha swala na kutoa sadaka. SURAH FATIR 35 Aya ya 29 - 30 SHEIKH ZAILAI H. B. MKOYOGORE SHEIKH WA WILAYA YA TEMEKE Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakasimamisha Swala, na wakatoa kwa siri na kwa uwazi katika tuliyowapa, wanataraji biashara isiyoangamia.

Ili awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila Zake. Hakika Yeye ni Mwingi wa maghufira, Mwenye shukrani.