Hakika hamuwezi kuwatosheleza watu kwa mali zenu,Basi watoshelezeni kwa tabia zenu
Shekhe Abdallah I. Mtitu (Namba ya Utambulisho: A0003)
Sheikh wa wilaya ya Kigamboni
Masjid Noor (Kituo cha Afya Kigamboni)
Dar es Salaam, Kigamboni, Dar es salaam
Tanzania

Dua kwa ajili ya marehemu

Kadiri tunavyo ishi, tunajikuta tunapoteza wapendwa wetu. Tunalia na kuhuzunika na kumuuliza Allah kwanini wapendwa wetu wametuacha. Na mara nyingine tunapoteza matumaini lakini dua kwa ajili ya waliokufa ni moja ya njia mojawapo ya kuendeleza matendo mema mpaka siku ya kiama . Majibu na faraja ya maumivu yetu yanapatikana kwa kuswali.