Umoja upendo na huruma ndiyo msingi wa mafanikio yetu
Shekhe Adam Y. Mwinyipingu (Namba ya Utambulisho: A0004)
Sheik wa wilaya ya ilala
Ofisi ya bakwata wilaya ya ilala (Ofisi ya bakwata wilaya ya ilala)
Dar es Salaam, Ilala, Dar es salaam
Tanzania

Sheikh Adam Mwinyipingu - Personal Certificate (Kiswahili)

Assalaam Aleykum

Ndugu yangu katika Imani hakuna kitu chenye thamani katika maisha yako kama
Imani, Imani itakujengea uwezo wa kumudu mazingira unayoishi katika maisha yako ya kila siku. Unapoishi hapa duniani ndio unatengeneza maisha yako ya baadae.
Jenga ukaribu na Mungu, kuwa rafiki mwema wa nafsi yako, ishi vyema na
wenzio tunza mazingira kupitia Imani yako ili ufahamu kiwango cha Imani yako.

8:2 Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao
hujaa hofu, na wanaposomewa Aya Zake huwazidisha imani, na wanamtegemea
Mola Wao.
8:3 Ambao wanasimamisha Swala na wanatoa katika yale tuliyowaruzuku.
8:4 Hao kweli ndio waumini; wao wana vyeo kwa Mola Wao, na maghufira na
riziki bora.
(SURA AL-ANFAL 8:2-4)