Kwa Mungu hakuna lisilowezekana
Askofu Sylvester S. Gamanywa (Namba ya Utambulisho: R0001)
Askofu
BCIC Mbezi Beach (Mbezi Juu)
Dar es Salaam, Kinondoni, Dar es salaam
Tanzania

Askofu Sylvester S. Gamanywa - DHIKI KUU DUNIANI

Tafsiri Ya Dhiki Kuu
Kwa mujibu wa Kamusi ya Biblia, neno dhiki kwa kiyunani ni thlipsis likiwa na maana ya kubanwa kwa maumivu makali, kukamuliwa
kama dhabibu, yote yakiwa na maana ya adha na mateso makali. Msamiati wa neno “dhiki kuu” umetajwa katika Agano Jipya na Yesu mwenyewe pale alipokuwa akitabiri kuhusu matukio makubwa yatakayoipata Israeli na dunia katika siku za mwisho. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba “dhiki kuu” ni kipindi maalum kinachokuja mbeleni ambacho Bwana anakusudia kutimiza mambo mawili katika mpango wake hapa duniani. Kwa mujibu wa nabii za Kibiblia kwa nyakati za mwisho, kipindi cha dhiki kuu kimetabiriwa kuwa ni miaka saba kamili, lakini yenye awamu kuu mbili ya utekelezaji wake.

Awamu ya kwanza imetabiriwa kuchukua muda wa miaka mitatu na nusu. Hii itakuwa ni awamu ambayo Mpinga Kristo anaimarisha utawala wake baada ya kufanya mkataba wa amani na Israeli. Sehemu ya pili na ya mwisho ya “dhiki kuu” nayo pia ni miaka mitatu na nusu.
Awamu hii ndiyo imebeba uzito wa msamiati huu wa “dhiki kuu” ambayo imetabiriwa kuwa kali na ya uharibifu mkubwa kupita dhiki zote zilizowahi kuwepo duniani na kwamba haitakuwepo tena baada ya hiyo. Kama nilivyodokeza awali ya kwamba, Yesu Kristo ndiye wa kwanza kutabiri habari za dhiki kuu na akaihusisha na “chukizo la uharibu” litakalosababishwa na utawala wa Mpingakristo katika
kipindi hicho: