DUNIA NI MAPITO TUSIHADAIKE NAYO
Shekhe Mohamad A. Muhenga (Namba ya Utambulisho: A0006)
Sheikh wilaya ya kinondoni
Masjid Mwembechai (karibu ya shule ya msingi mwalimu Nyerere.)
Dar es Salaam, Kinondoni, Dar es salaam
Tanzania

Sheikh Mohamad Muhenga - Cheti Binafsi (Kiswahili)

Ndugu yangu usihaidaike na maisha ya duniani kwa kupotoshwa na mali, familia, mke/mume, watoto au cheo kwani vitu vyote hivyo ni vitu vya kuazimwa unaweza kuvipata ukavimiliki lakini tambua uko mwaka, mwezi, siku au saa yoyote unaweza ukaviacha au vikakuacha. Kinachotakiwa ni kumcha mwenyezi Mungu na kumuweka mbelekwa kila kitu kwani yeye ndiye mwenye kukujalia ukapata vyote vizuri uvipendavyo.

Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na upuzi, na pambo, na kujifaharisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Ni kama mfano wa mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukaiona ina rangi ya njano kisha ikawa makapi. Na Akhera kuna adhabu kali na maghufira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi.
Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.
Kimbilieni maghufira ya Mola Wenu, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyowekewa waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.