Hapana maisha mazuri na ya kudumu ila maisha ya akhera.
Shekhe Juma S. Muyenga (Namba ya Utambulisho: D0002)
Sheikh
Faith an madina (Ospital ya dr hameer)
Dar es Salaam, Ilala, DSM
Tanzania

Juma Sadiki Muyenga - Cheti Binafsi (Kiswahili)

Assalaam Aleykum

Anasema Allah Mtukufu katika Quran sura 18: aya 10 na aya 22. hakika aya hizi zinaonyesha namna mwenyezi Mungu alivyompandisha Mbwa daraja kwa Sababu ya kushirikiana na kuwapenda watu wema, kapewa hadhi kama binaadamu na hakika ataingia nao peponi inshaAllah.

Watasema ni watatu na wanne wao ni mbwa wao. Na wa nasema ni watano na wa sita wao ni mbwa wao, kwa kuvurumisha ya ghaibu. Na wanasema ni saba na wanane wao ni mbwa wao. Sema, Mola Wangu ndiye anayejua zaidi idadi yao. Hawawajui isipokuwa wachache. Basi usibishane juu yao isipokuwa mabishano ya juu juu; wala usiulize habari zao kwa yeyote yule.