Mambo matatu yakikupita hayarudi :wakati,ujana,na uzuri.Basi jitunze vizuri.
Shekhe Ally M. Mkoyogore (Namba ya Utambulisho: D0004)
Naibu Kadh mkuu
Masjid Kadiria. (karibu na Temeke hospital.)
Dar es Salaam, Temeke, DSM
Tanzania

Dua kwa ajili kujaliwa uzazi

Mara nyingine watu wanapata shida kupata watoto na kila mara wanahama kutoka kwa daktari mmoja kwenda kwa daktari mwingine kutafuta ushauri ya jinsi ya kushika mimba. Wengine hutumia njia za kienyeji lakini hawafanikiwi. Watoto ni Baraka kutoka kwake Allah . Allah ndie anayetupa uhai Wakati wanandoa wanahangaika kupata watoto, ni muhimu Allah kuingilia kati.