Kama sio Mimi, nani? Kama sio sasa lini?
Monalisa . (Namba ya Utambulisho: Y0003)
Actress /producer
common.leader.title.-1 Monalisa . (Namba ya Utambulisho: Y0003)
Actress /producer

Ujumbe Binafsi

Nelson Mandela aliwahi kusema kwamba katika maisha jambo lililo na maana zaidi si kuishi tu. Bali ni utofauti tunaouwezesha kutokea katika maisha ya wengine ndio
unaongeza maana katika maisha tunayoishi. Binafsi naguswa na maneno haya na naamini tuko hapa duniani kwa makusudio makubwa zaidi ya kutafuta ili kupata kile
tunachokitaka katika maisha. Makusudio hayo kwangu ni kuona Wanawake na Watoto ambao ni waathirika wa vitendo mbali mbali dhalili katika jamii yetu, majanga ya asili,
ajali na wale wanaozaliwa wakiwa na changamoto mbali mbali za kimaumbile wanapata fursa ya kutabasamu tena. Huo ndio utofauti ninaoutamani kuuona unatokea. Tafadhali jumuika nami.

SADAKA NETWORK,AGAKHAN NA HOPITAL YA MUHIMBILI KUUNGANA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA
Nov 08, 2018

Nelson Mandela aliwahi kusema kwamba katika maisha jambo lililo na maana zaidi si kuishi tu. Bali ni utofauti tunaouwezesha kutokea katika maisha ya wengine ndio unaongeza maana katika maisha tunayoishi. Binafsi naguswa na maneno haya na naamini tuko hapa duniani kwa makusudio makubwa zaidi ya kutafuta ili kupata kile tunachokitaka katika maisha. Makusudio hayo kwangu ni kuona Wanawake na Watoto ambao ni waathirika wa vitendo mbali mbali dhalili katika jamii yetu, majanga ya asili, ajali na wale wanaozaliwa wakiwa na changamoto mbali mbali za kimaumbile wanapata fursa ya kutabasamu tena. Huo ndio utofauti ninaoutamani kuuona unatokea. Tafadhali jumuika nami. Soma Zaidi...

SADAKA NETWORK,AGAKHAN NA HOPITAL YA MUHIMBILI KUUNGANA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA
Nov 08, 2018

Watanzania wameombwa kwa pamoja kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya SADAKA NETWORK , Hospitali ya Muhimbili na Aga Khan kwa kushirikiana na Women to women foundation kuchangia kurudisha tabasamu usoni kwa wakina mama na watoto waliopata matatizo hayo kwa bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia, kupigwa au matatizo yoyote yaliyopelekea wao kuharibika maumbile yao ikiwa ni usoni ama sehemu nyengine ya mwili. Mwanzilishi wa taasisi hiyo Dkt. Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa gharama za kuwatibu watoto na akina mama ni kubwa na haziwezi kubebwa na Muhimbili au Aga Khan peke yake wala Women to women foundation,bali ghalama hizi zitafanikiwa endapo wananchi wataungana kwa pamoja ili kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi hilo. "Upasuaji huu utafanyika katika Hospitali ya Muhimbili na Aga Khan na tunatarajia kuwafanyia upasuaji watu 40 kutoka sehemu zote Tanzania,hivyo pesa inayohitajika ni Tsh Milioni 268" alisema Dkt. Msengi. http://www.mwanaharakatimzalendo.co.tz/2018/11/taasisi-ya-sadaka-networkhospitali-ya.html Soma Zaidi...

Jiandikishe bure

Wafuasi

Changia mradi ya jumuiya

CHANGIA

Onyesha huduma zote

Huduma zote