Fanya utakavyo, kama ufanyavyo ndivyo utakavyolipwa
Alhad M. Salum (Namba ya Utambulisho: A0002)
Sheikh wa mkoa wa dar es salaam

Dua ya kujalia mafanikio ya elimu

Mtume wa Allah alisema ‘’kuitafuta elimu ni jukumu la kila Muislam. Elimu ni ufunguo wa maisha. Kwa sababu hii, wazazi wanafanya kazi kwa bidii ilikuweza kupeleka watoto wao shule na pia watu wazima wanajiendeleza kielimu kwa kusoma masomo ya elimu ya juu ili kuweza kuongeza mwanga kwenye kazi zao. Hata hivyo, elimu haitakuwa na maana endapo Allah atasahaulika. Ili kuweza kufanikiwa katika elimu, mtu anahitaji muongozo wa Allah ili afanye uchaguzi sahihi wa kazi.