Fanya utakavyo, kama ufanyavyo ndivyo utakavyolipwa
Alhad M. Salum (Namba ya Utambulisho: A0002)
Sheikh wa mkoa wa dar es salaam

Dua ya kujalia mafanikio maishani

Wote tunatamani maisha mazuri na tunatamani kupata mahitaji muhimu katika maisha kama chakula, malazi afya njema na elimu. Licha ya hayo, maisha yana changamoto nyingi ambazo zinasababisha umasikini, magonjwa na kuleta woga kuhusu kesho ( siku zinazokuja). Quran inasema” Allah aliahidi wingi wa msamaha kutoka kwake” ( 7:188) . Tunahitaji muongozo kutoka kwa Allah ilikuweza kuchuma na kufurahia mahitaji muhimu ya ya maisha.