Wakati ujao ni bora zaidi kwako kuliko wakati uliopo
Shekhe Hilali S. Makarani - Kipozeo (Namba ya Utambulisho: D0001)
Sheikh wa al Marid islamic former centre
Nyumbani kwake (Karibu na msikiti wa juhudi mchangani)
Dar es Salaam, Kinondoni, DSM
Tanzania

Shekhe Hilali Makarani (Kipozeo) - Cheti Binafsi (Kiswahili)

Asalam aleykum warahmatullah wabarakat, Alhamdulillah waswalatu wasalam Allah rasulillah (S.W) wabaat. Baada ya kumshukuru Mwenyezimungu Subhanau wataallah, na baada ya kumtakia rehma kiongozi wa Uma huu, bwana Mtume Mohamad (S.W), ni mimi ndugu yako kwa jina naitwa SHEIKH KIPOZEO, ni ndugu yako katika Imaani na ni ndugu wa damu nikisema ndugu yako katika Imaani ukiwa wewe ni muislam, lakini ukiwa sio Muislam mimi ni ndugu yako wa damu, kwa mara nyingine tena tunatoa cheti binafsi kwa Yule yoyete atakae jisajili na kujiunga kwaajili ya kusikiliza mawaidha yetu basi mimi binafsi nitampa zawadi ya cheti bure atakachokipata kwenye simu yake baada ya kuwa kashajisajili katika hii Sadaka Network, na humo katika cheti utapata faida ndani yake kutakua na Risala risala maanayake ni ujumbe mfupi ambao utakupa faida wewe katika maisha yako. Asalam aleykum warahmatullah wabarakat.